Skip to content

Arsenal wajiondoa kwenye usajili wa Jeremy Monga, Manchester City wanasonga mbele

SokaNews
Updated: Published: Alhamisi, 2 Julai 2026 · 2 min read
arsenal manchestercity jeremymonga usajili premierleague leicestercity
Arsenal wajiondoa kwenye usajili wa Jeremy Monga, Manchester City wanasonga mbele

Arsenal wajitoa kumsajili Jeremy Monga

Klabu ya Arsenal imethibitisha kujiondoa katika mbio za kumsajili winga kijana na mwenye kipaji kikubwa, Jeremy Monga, anayetokea Leicester City. Hatua hii imekuja baada ya taarifa kuonyesha kuwa Manchester City wapo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 16.

Awali, ilionekana kama Arsenal wamefanikiwa kumpata kijana huyo baada ya kuripotiwa kuwa alikuwa amewachagua ‘The Gunners’ mbele ya vilabu vingine vikubwa vilivyokuwa vikimwinda. Hata hivyo, hali imebadilika ghafla na sasa anaonekana kuelekea Etihad.

Kwanini Arsenal wameshindwa?

Kuna sababu kadhaa zilizochangia Arsenal kushindwa kufikia muafaka wa kumsajili Monga. Kwa mujibu wa ripoti kutoka kwa wachambuzi mbalimbali, tofauti ya bei ilikuwa kikwazo kikubwa. Arsenal walikuwa tayari kutoa kiasi cha pauni milioni 6.5, wakati Leicester City walikuwa wakiitaji kiasi kisichopungua pauni milioni 10 hadi 12.

Manchester City, kwa upande wao, wameingilia kati na wako tayari kutoa kiasi kinachokadiriwa kufikia pauni milioni 10, jambo ambalo limeonekana kumshawishi klabu ya Leicester kukubali ofa hiyo.

Ushawishi wa Enzo Maresca

Sababu nyingine iliyomfanya Monga kubadili mawazo ni ushawishi wa kocha mpya wa Manchester City, Enzo Maresca. Inafahamika kuwa Maresca anayemfahamu vyema kijana huyo tangu alipokuwa akiifundisha Leicester City, amekuwa na nafasi kubwa katika kumshawishi mchezaji huyo kujiunga na mradi wake mpya.

Fabrizio Romano amebainisha kuwa mipango na maono aliyomweleza Monga yamebadili mwelekeo wa mchezaji huyo. Kwa sasa, Arsenal wameonekana kukata tamaa kabisa na kujiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho, huku dili likitarajiwa kukamilika wakati wowote kuanzia sasa.

Usajili huu unaendelea kuleta changamoto kwa Arsenal katika dirisha hili, kwani wamekuwa wakikumbana na vikwazo katika jitihada zao za kuimarisha kikosi, ikiwemo harakati za kumsaka Bruno Guimaraes ambaye Newcastle United hawapo tayari kumuuza.