Barcelona na Atletico Madrid zatingira nyota wa Tottenham
Tottenham katika harakati za kupunguza kikosi
Klabu ya Tottenham Hotspur inaendelea kuwa na shughuli nyingi katika dirisha hili la usajili, lakini sasa nguvu zimeanza kuelekezwa katika kupunguza idadi ya wachezaji ili kuweka uwiano sawa wa kifedha. Baada ya kufanya usajili wa wachezaji sita wapya, ikiwemo Sandro Tonali na Andy Robertson, sasa ni zamani za baadhi ya nyota kuondoka klabuni hapo.
Cristian Romero karibu na Atletico Madrid
Beki kisiki Cristian Romero anaonekana kuwa ndiye mchezaji aliye karibu zaidi na mlango wa kutokea. Ripoti kutoka Hispania kupitia Cadena Ser zinaeleza kuwa Atletico Madrid wameongeza kasi ya mazungumzo ili kukamilisha usajili wake.
Inaelezwa kuwa Atletico wapo katika nafasi nzuri zaidi dhidi ya klabu nyingine kama Arsenal, Barcelona na Inter Milan. Uhamisho huu unatazamiwa kukamilika ndani ya siku chache zijazo kwa ada inayokadiriwa kufikia Euro milioni 40.
Barcelona yajipanga kwa Pedro Porro
Katika tukio jingine, Barcelona wameripotiwa kuanza mawasiliano na wawakilishi wa beki wa pembeni Pedro Porro. Mwandishi Gerard Romero amedai kuwa Barcelona wanamtazama Porro kama mrithi sahihi ikiwa Jules Kounde ataondoka klabuni hapo.
“Mawasiliano yamefanyika siku za hivi karibuni na Pedro Porro pamoja na wawakilishi wake. Yeye ni mmoja wa wachezaji wanaolipwa vizuri Tottenham, lakini Barcelona wanahakiki uwezekano huo iwapo Kounde ataamua kuondoka,” alisema Romero.
Hata hivyo, Porro si chaguo la Barcelona pekee; Manchester City nao wamekuwa wakifuatilia kwa karibu hali ya mchezaji huyo, ingawa inasemekana kuna tofauti kubwa ya bei inayotakiwa na Tottenham kulinganisha na kile klabu hizo zinachotarajia kutoa.
Djed Spence naye yumo
Kando na wakubwa hao, Djed Spence naye anaonekana kuwa njiani kuelekea Inter Milan. Mtaalamu wa masuala ya usajili Fabrizio Romano amethibitisha kuwa Inter wapo kwenye mazungumzo ya moja kwa moja na Tottenham ili kumsajili beki huyo wa kulia.
Spence mwenyewe anatajwa kuwa tayari kwa changamoto hiyo mpya nchini Italia, huku maamuzi ya mwisho yakibaki mikononi mwa Tottenham kuhusu masharti ya dili hilo. Kwa sasa, mashabiki wa Spurs wanasubiri kuona ni nani atakayeondoka rasmi kabla ya dirisha kufungwa.