Jamie Carragher amchana Alexis Mac Allister baada ya tamko lake klabuni Liverpool
Ujumbe mzito wa Carragher kwa Mac Allister
Alexis Mac Allister huenda alikuwa shujaa wa usiku wa Liverpool katika mchezo wao dhidi ya Atletico Madrid baada ya kufunga bao la ushindi, lakini si kila mtu anayempongeza kwa moyo mmoja. Legend wa Liverpool, Jamie Carragher, ameweka wazi kuwa bado hajamsamehe kiungo huyo kwa kauli zake za hivi karibuni kwenye mkutano na waandishi wa habari.
Katika mkutano huo, Mac Allister alieleza wazi kusikitishwa kwake na kutopewa mkataba mpya na klabu hiyo, huku akidai kuwa alikuwa na chaguzi nyingine za kuondoka wakati wa dirisha la usajili la majira ya kiangazi. Maneno haya yaliwakasirisha mashabiki wengi wa ‘The Reds’ ambao wanaamini kiwango chake kilishuka sana msimu uliopita.
”Haikuwa sawa”
Akizungumza kwenye CBS Sports, Carragher alikiri kuwa bao la Mac Allister lilikuwa muhimu, lakini hilo halifuti ukweli kuwa kiungo huyo alikosea kutumia jukwaa la vyombo vya habari kulalamika kuhusu mkataba wake.
“Mac Allister, ambaye alizungumza mengi jana, leo amejibu kwa vitendo uwanjani. Hata hivyo, hilo halifanyi kile alichokifanya jana kwenye mkutano na waandishi wa habari kuwa sahihi. Ingawa sasa ataonekana kwa sura nzuri zaidi baada ya kufunga bao la ushindi,” alisema Carragher.
Ushauri wa Steven Gerrard
Kwa upande mwingine, mkongwe Steven Gerrard alionekana kuvutiwa na kiwango cha mchezaji huyo uwanjani, akimtaka ajikite zaidi kwenye soka badala ya mambo ya nje ya uwanja. Gerrard anaamini kuwa njia pekee ya Mac Allister kupata mkataba mpya ni kuonyesha kiwango cha juu mara kwa mara.
“Nadhani kiwango chake kimekuwa bora sana. Acha soka lako ndilo lizungumze. Consistency, kiwango cha juu, na uzoefu—hivi ndivyo vitakavyoifanya klabu ikuone unastahili mkataba mpya,” alisisitiza Gerrard.
Gerrard aliongeza kuwa wakati wa Mac Allister kuongelea mkataba wake ulikuwa mbaya na haukusaidia chochote. Kwa mtazamo wake, mambo kama hayo yanapaswa kuzungumzwa faraghani na kocha, sio kupitia vyombo vya habari ambavyo huleta presha isiyo ya lazima kwa timu.