Chelsea wamnyemelea staa wa Arsenal katika dakika za mwisho za usajili
Chelsea katika pilikapilika za mwisho
Klabu ya Chelsea imejikuta katika shinikizo kubwa ya kutafuta kiungo mpya kabla ya dirisha la usajili kufungwa. Hali hii inakuja huku kukiwa na taarifa za uwezekano wa kiungo wao, Enzo Fernandez, kutimkia Manchester City, jambo linalowalazimu mabosi wa Stamford Bridge kutafuta mbadala wa haraka.
Ripoti za kuaminika zinaonyesha kuwa Chelsea wamepania kuimarisha safu yao ya kiungo kwa kumtazama staa wa Arsenal, Martin Zubimendi, kama mbadala sahihi. Hii inakuja baada ya jitihada zao za kumsajili Lamine Camara kutoka Monaco kukwama, baada ya ofa yao ya pauni milioni 38.5 kukataliwa.
Liverpool watajwa kumvizia Camara
Mambo yameonekana kuwa magumu kwa Chelsea kumpata Camara, huku kukiwa na minong’ono kuwa nyota huyo anaweza kusubiri hadi msimu ujao ili kutua Liverpool. Inadaiwa kuwa Liverpool wameonyesha nia ya kumsajili kiungo huyo, lakini hawatofanya haraka katika dirisha hili la usajili.
Mwandishi wa habari za michezo, Ben Jacobs, amedai kuwa Camara huenda akalazimika kufanya maamuzi magumu kuhusu mustakabali wake. “Camara anaweza kukabiliwa na chaguo. Je, anasubiri Liverpool? Inawezekana kama Alexis Mac Allister ataondoka mwaka 2027, lakini kwa sasa Chelsea ndio wanaojaribu,” alisema Jacobs.
Majina mengine kwenye rada za Chelsea
Mbali na Zubimendi, Chelsea pia wamehusishwa na viungo wengine wanaocheza Ligi Kuu ya England (EPL). Majina yaliyotajwa ni pamoja na Lucas Bergvall wa Tottenham na Morgan Gibbs-White wa Nottingham Forest.
Ingawa bado hakuna ofa rasmi iliyowasilishwa kwa wachezaji hawa, wanatajwa kama sehemu ya orodha ya wachezaji wanaoweza kuziba pengo la Enzo Fernandez iwapo ataondoka. Hata hivyo, wataalamu wa soka wana mashaka juu ya uwezekano wa Arsenal kumuachia Zubimendi kwa urahisi.
Akizungumzia suala la Zubimendi, gwiji wa Arsenal, Martin Keown, alisema:
“Ninaweza kuona hilo likitokea, lakini kumbuka alicheza mchezo muhimu akitokea benchi hivi karibuni. Sioni Arsenal wakitaka kuvunja kikosi chao kwa sasa, amedumu msimu mmoja tu na alicheza michezo 57 mwaka jana. Itakuwa vigumu sana kwao kumruhusu aondoke.”
Kadhalika, Chelsea wamekuwa wakijaribu kumsajili Manu Kone kutoka Roma, lakini kocha wa klabu hiyo, Gian Piero Gasperini, amekuwa mgumu kumwachia mchezaji huyo licha ya mazungumzo ya pauni milioni 52 kuendelea.