Skip to content

JJ Gabriel kuelekea mlango wa kutokea Manchester United

SokaNews
Updated: Published: Jumapili, 20 Septemba 2026 · 2 min read
manchesterunited jjgabriel usajili michaelcarrick sokalaulaya
JJ Gabriel kuelekea mlango wa kutokea Manchester United

Hatima ya JJ Gabriel Man Utd yazua mjadala

Manchester United wako katika hatari ya kumpoteza mmoja wa chipukizi wao wenye kipaji kikubwa zaidi, JJ Gabriel. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 15, ambaye anatarajiwa kutimiza miaka 16 mwezi ujao, ameripotiwa kutoa uamuzi wa kuondoka klabuni hapo baada ya kutokea kutoelewana kati yake na familia yake na uongozi wa klabu hiyo.

Gabriel, ambaye amepewa jina la utani la ‘Kid Messi’ kutokana na uwezo wake mkubwa uwanjani, alikuwa mfungaji bora wa kikosi cha Under-18 msimu uliopita na alikisaidia kikosi hicho kufika fainali ya FA Youth Cup. Ripoti zinaeleza kuwa anaweza kuondoka Old Trafford ndani ya wiki chache zijazo.

Vilabu vikubwa Ulaya vinyatia saini yake

Taarifa zinaeleza kuwa mchezaji huyo anapendelea kuendeleza soka lake nje ya Uingereza badala ya kujiunga na klabu nyingine ya Ligi Kuu ya Uingereza (Premier League). Vilabu vikubwa kama Barcelona, Real Madrid, Bayern Munich, na PSG vimehusishwa sana na kutaka huduma yake.

Licha ya kuwepo kwa tetesi za kusafiri kuelekea Hispania kwa mazungumzo na Barcelona, mwandishi wa habari za usajili, Fabrizio Romano, amewataka wadau kuwa watulivu kwa sasa:

“Hiyo ndiyo hali ilivyo kwa sasa, mazungumzo yapo, lakini mchezaji hajasafiri kwenda kuzungumza na Barcelona. Kwa sasa anasubiri kuona ni klabu gani itakuwa chaguo bora kwa ajili ya maisha yake ya baadaye. Tutaona nini kitatokea katika wiki zijazo.”

Ujumbe wa Michael Carrick kwa chipukizi

Katika upande mwingine, kocha Michael Carrick amezungumzia umuhimu wa kulea vipaji kutoka akademi ya klabu hiyo. Ingawa hakuzungumza moja kwa moja kuhusu suala la Gabriel, sifa alizozitoa kwa chipukizi mwenzake, Shea Lacey, zimechukuliwa kama ujumbe wa wazi kwa vijana wanaopata fursa ya kuitumikia Man Utd.

Akizungumza kuhusu Lacey, Carrick alisema:

“Ni jambo la ajabu kwa Shea, familia yake, na kila mtu aliyehusika na akademi. Ni fahari kuona kijana akianzia safari yake na kupata nafasi ya kuanza mchezo Old Trafford. Hiyo ndiyo historia ya klabu hii, ni sehemu ya uchawi na uzuri wa klabu hii.”

Kwa sasa, mashabiki wa United wanasubiri kuona kama klabu itaweza kumbadilisha mchezaji huyo maamuzi yake au kama atakuwa ni mmoja wa vipaji vitakavyoondoka mapema kutafuta changamoto mpya nje ya nchi.