Skip to content

Joe Cole atabiri Real Madrid kubeba Champions League msimu huu

SokaNews
Updated: Published: Jumatano, 9 Septemba 2026 · 2 min read
realmadrid arsenal championsleague josemourinho joecole
Joe Cole atabiri Real Madrid kubeba Champions League msimu huu

Real Madrid wana nafasi kubwa, asema Joe Cole

Wakati takwimu za Opta zikiwapa Arsenal nafasi kubwa zaidi ya kutwaa taji la UEFA Champions League msimu huu, kiungo wa zamani wa Chelsea na timu ya taifa ya England, Joe Cole, ana mtazamo tofauti.

Cole ameweka pembeni utabiri unaoibeba Arsenal na badala yake amemchagua Jose Mourinho kuwa ndiye kocha atakayeiongoza Real Madrid kunyakua ubingwa huo wa Ulaya. Utabiri huu unakuja wakati ambapo Real Madrid wamemrejesha Mourinho kwa mara ya pili kikosini ili kurekebisha mambo.

Hadithi ya ‘Hollywood’ ya Mourinho

Akizungumza na TNT Sports, Cole anaamini kuwa Mourinho bado ana uwezo mkubwa wa kufanya maajabu, hususan anapokuwa na wachezaji wa daraja la juu. Kwa mujibu wa Cole, kuna mazingira yanayochochea mafanikio kwa Madrid msimu huu.

“Mtu huyu ni kama hadithi ya filamu za Hollywood. Naimani anaweza kulifanya hilo. Watu wengi wamemtoa kwenye hesabu, lakini nadhani bado ni kocha wa kiwango cha juu kabisa na anaendana vyema na wachezaji wenye vipaji vikubwa,” alisema Cole.

Cole anaongeza kuwa ukweli kwamba fainali ya msimu huu inatarajiwa kupigwa kwenye uwanja wa mahasimu wa Real Madrid, yaani Atletico Madrid, kunafanya kila kitu kuonekana kama filamu ya kusisimua.

Changamoto ya Mbappe na Vinicius

Licha ya imani hiyo, Cole anakiri kuwa kuna changamoto ambazo Mourinho anapaswa kuzitatua ili kufikia malengo hayo. Miongoni mwa mambo hayo ni kuhakikisha Kylian Mbappe anaanza kucheza katika ubora wake na kuifanya timu izunguke kumzunguka yeye. Pia, kubaki kwa Vinicius Jr ndani ya klabu hiyo kumeonekana kuwa hatua muhimu sana kwa mafanikio yao.

“Kitu pekee wanachopaswa kukimaliza ni swala la Kylian Mbappe, wakifanikiwa kumfanya afunge na timu ikacheza kwa ushirikiano, basi watafika mbali. Kubaki kwa Vinicius ilikuwa hatua kubwa kwa klabu,” aliongeza Cole.

Arsenal na matumaini yao

Kwa upande wa Arsenal, msimu huu wanatazamwa kama tishio kubwa barani Ulaya. Baada ya kumaliza ukame wa miaka 22 bila taji la Premier League msimu uliopita, vijana wa Mikel Arteta wameimarisha kikosi chao kwa kusajili wachezaji kama Bruno Guimaraes, Ezri Konsa, na Christos Tzolis.

Ingawa Opta inawapa Arsenal asilimia 20.4 ya kushinda taji hilo ikilinganishwa na asilimia 5.1 ya Real Madrid, Cole anaamini kuwa uzoefu na mbinu za Mourinho ndizo zitakazoamua hatma ya taji hilo mwishoni mwa msimu.