Skip to content

Jules Kounde bado anataka kubaki Barcelona, Arsenal wamepata kigugumizu

SokaNews
Updated: Published: Jumanne, 11 Agosti 2026 · 2 min read
arsenal barcelona juleskounde usajili ligikuu sokalaulaya
Jules Kounde bado anataka kubaki Barcelona, Arsenal wamepata kigugumizu

Arsenal wanatafuta mbadala wa Saliba

Klabu ya Arsenal inaendelea na mikakati mizito katika dirisha hili la usajili huku lengo kuu likiwa ni kuimarisha safu ya ulinzi. Hii inafuatia taarifa za majeraha ya muda mrefu yanayomkabili beki wao kisiki, William Saliba, jambo ambalo limemlazimisha kocha Mikel Arteta kutafuta mchezaji mwingine mwenye uwezo wa kucheza nafasi ya beki wa kati na hata beki wa kulia.

Kounde ni chaguo la Arteta, lakini…

Miongoni mwa majina yanayotajwa sana ni beki wa kimataifa wa Ufaransa, Jules Kounde, anayekipiga Barcelona. Kwa mujibu wa ripoti kutoka nchini Hispania, Arsenal wameonyesha nia ya wazi ya kumtaka mchezaji huyo ambaye ana uwezo mkubwa wa kucheza nafasi mbalimbali za ulinzi, jambo ambalo ni hitaji muhimu kwa Arteta.

Barcelona inaelezwa kuwa iko tayari kusikiliza ofa za mamilioni ya pesa ili kumwachia Kounde, hatua inayolenga kuipatia klabu hiyo fedha za kuimarisha maeneo mengine ya kikosi chao chini ya kocha mpya, Hansi Flick. Hata hivyo, mpango huu unaweza kukwama kutokana na msimamo wa mchezaji mwenyewe.

Mchezaji anataka kubaki Camp Nou

Licha ya uvumi huo, Kounde bado ana nia ya kuendeleza maisha yake katika klabu ya Barcelona. Ripoti zinaeleza kuwa mchezaji huyo ameweka wazi mipango yake ya kubaki, ingawa hali inaweza kubadilika kulingana na mazungumzo yake na kocha Hansi Flick.

“Chaguo la Kounde linamvutia Arteta, ingawa maendeleo yamekwama kwa sasa, kwani mchezaji huyo hivi karibuni aliongeza mkataba wake na Barcelona na kila kitu kinaashiria kuwa anataka kubaki klabuni hapo.”

Ripoti hiyo inaongeza kuwa bado kuna sintofahamu kwani Barcelona inahitaji kufanya marekebisho kwenye safu yao ya ulinzi na kupata fedha, hivyo Kounde anaweza kuonekana kama mchezaji anayeweza kuleta mapato makubwa.

Nani wengine wako kwenye rada za Arsenal?

Arsenal haijajikita kwa Kounde pekee. Klabu hiyo imekuwa ikihusishwa na beki wa Aston Villa, Ezri Konsa, ingawa kuna mgongano mkubwa wa bei kati ya klabu hizo mbili. Wakati Villa wakitaka kiasi cha paundi milioni 60, Arsenal inaonekana kuwa tayari kutoa kiasi kinachokaribia paundi milioni 40.

Aidha, kumekuwa na mazungumzo kuhusu Cristian Romero wa Tottenham, lakini ushindani na uhasama wa klabu hizo za London Kaskazini unafanya dili hilo kuwa gumu, huku beki Jacobo Ramon naye akitajwa kuwa kwenye orodha fupi ya Arsenal.