Liverpool yageukia nyota wa Chelsea na Man City baada ya dili la Diomande kukwama
Liverpool yabadili upepo sokoni
Klabu ya Liverpool inaendelea na msako mkali wa kumpata mshambuliaji mpya wa pembeni kufuatia hali ya sintofahamu inayomkabili nyota wao, Mohamed Salah, ambaye anahusishwa na uwezekano wa kuondoka klabuni hapo msimu huu.
Baada ya kufanikiwa kumsajili Victor Munoz kutoka Osasuna, kocha mpya Andoni Iraola anaonekana bado hajaridhika na kikosi chake na anahitaji nguvu zaidi katika eneo la ushambuliaji. Hata hivyo, mipango ya awali ya kumsajili staa wa RB Leipzig, Yan Diomande, imepata pigo baada ya mchezaji huyo kuonyesha nia ya kutaka kujiunga na PSG badala ya kutua Anfield.
Macho kwa Neto na Savinho
Kutokana na ugumu wa kumpata Diomande na bei ya juu ya Bradley Barcola kutoka PSG, Liverpool wameamua kuangalia chaguzi nyingine ndani ya Ligi Kuu ya Uingereza (Premier League). Ripoti mpya kutoka kwa mwandishi Dave Davis zinaonyesha kuwa majogoo hao wa Anfield wamefanya mawasiliano rasmi kuhusu uwezekano wa kuwasajili Pedro Neto wa Chelsea na Savinho wa Manchester City.
Akizungumzia hali ya Neto, Davis alisema:
Liverpool wanaonekana kurejea kwenye ushirikiano na wakala Jorge Mendes, ambaye anamsimamia Pedro Neto. Ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa wa kupiga krosi na ana sifa za kipekee kama mchezaji anayeweza kusafirisha mpira na kuingia kwenye hatari.
Inaripotiwa kuwa Neto mwenyewe anaweza kuvutiwa sana na ofa ya kujiunga na Liverpool, ikizingatiwa kuwa klabu hiyo ilishawahi kuhusishwa na mpango wa kumsajili wakati akiwa Wolverhampton Wanderers miaka ya nyuma.
Uchambuzi kuhusu Savinho
Kuhusu Savinho wa Manchester City, Liverpool wanaonekana kuvutiwa na uwezo wake wa kupambana na mabeki (progressive carries). Hata hivyo, wachambuzi wameonya kuwa licha ya kasi yake, mchezaji huyo bado ana mapungufu katika kutengeneza nafasi za mabao, jambo ambalo ndilo lililomfanya mara nyingi kuanzia benchi chini ya Pep Guardiola msimu uliopita.
Davis aliongeza kwa tahadhari:
Tunapozungumzia Savinho, ni mchezaji mahiri sana anapokuwa na mpira miguuni mwake. Hata hivyo, ukiondoa uwezo wake wa kukimbia na mpira, bado hajatengeneza nafasi nyingi za mabao. Kuna sababu kwanini alikuwa akikaa benchi mara nyingi msimu uliopita.
Kwa sasa, Liverpool wanaonekana kuwa katika kipindi cha mpito wakitafuta mbadala sahihi wa kuziba nafasi za washambuliaji wao, huku mashabiki wakisubiri kuona ni nani atakayekuwa chaguo la mwisho la uongozi wa klabu hiyo.