Skip to content

Liverpool yajipanga kunasa saini ya Bradley Barcola kutoka PSG

SokaNews
Updated: Published: Jumanne, 18 Agosti 2026 · 2 min read
liverpool bradleybarcola psg usajili ligikuu
Liverpool yajipanga kunasa saini ya Bradley Barcola kutoka PSG

Liverpool mbioni kukamilisha dili la Barcola

Klabu ya Liverpool inaendelea na mikakati mizito ya kumsajili winga wa Paris Saint-Germain (PSG), Bradley Barcola. Licha ya awali kuwa na changamoto katika mazungumzo, taarifa za karibu zinaeleza kuwa dili hilo linaweza kukamilika hivi karibuni.

Baada ya kumsajili Victor Munoz kutoka Osasuna mapema msimu huu, Liverpool bado inaonekana kuhitaji kuongeza nguvu katika nafasi ya ushambuliaji ili kuziba pengo la muda mrefu la Mohamed Salah. Barcola ndiye anayeonekana kuwa chaguo namba moja la klabu hiyo kwa sasa.

Mkakati wa kusubiri bei kushuka

Mchambuzi wa mambo ya soka, Ben Jacobs, amedokeza kuwa Liverpool wanatumia mbinu ya kusubiri ili kuishinikiza PSG kupunguza bei ya mchezaji huyo. PSG, ambayo imeongeza nyota kama Ferran Torres na wengine kikosini, inatajwa kuwa tayari kumuuza Barcola ili kupunguza msongamano wa wachezaji.

“Ikiwa Liverpool watasubiri na kusubiri, wanahisi nafasi ya Barcola itakuwa ngumu kwasababu PSG wamewasajili Ferran Torres, Mika Godts na Maghnes Akliouche,” alisema Jacobs kupitia talkSPORT.

Je, Barcola anataka kuhamia Arsenal?

Kumekuwa na minong’ono mitandaoni ikidai kuwa nyota huyo angependelea kujiunga na Arsenal badala ya Liverpool. Hata hivyo, taarifa hizo hazijathibitishwa na klabu yoyote, na inaonekana Arsenal hawajatoa ofa rasmi inayokaribia kile ambacho PSG inakihitaji.

Kwa upande mwingine, mwandishi wa habari za Liverpool, David Lynch, anaamini kuwa mazungumzo yanaendelea vizuri na dili linaelekea kwenye hitimisho chanya.

“Mazungumzo yanaendelea. Nafikiri jambo linalofuata tutakalosikia ni kwamba dili limekamilika. Kila mtu anajua kinachoendelea. PSG wako tayari kuuza na Liverpool wako tayari kununua,” aliongeza Lynch kupitia podikasti ya Anfield Index.

Lynch alisisitiza kuwa hana hofu yoyote kuhusu dili hilo na anaamini Barcola atatua Anfield kabla ya dirisha la usajili kufungwa. Huku mchezaji mwenyewe akiripotiwa kutamani zaidi kucheza soka lake Liverpool, mashabiki wa klabu hiyo wanatarajia habari njema katika siku za usoni.