Paul Scholes aibua utata: Asema England ina wachezaji bora kuliko Hispania, amshambulia Thomas Tuchel
Scholes aibua mjadala mzito kuhusu England
Gwiji wa Manchester United, Paul Scholes, ametoa maoni mazito yaliyozua gumzo baada ya kumalizika kwa mashindano ya Kombe la Dunia. Katika maoni yake, Scholes amedai kuwa kikosi cha England kina wachezaji wenye vipaji bora zaidi binafsi ikilinganishwa na mabingwa wapya wa dunia, Hispania.
Ingawa kauli hiyo inaweza kuonekana ya kushangaza kwa mashabiki wengi, Scholes amesisitiza kuwa tatizo la England si ubora wa wachezaji, bali ni kukosa utambulisho wa timu. Anasema kuwa England imekuwa na wachezaji mahiri lakini wanacheza kwa ubinafsi.
“Naamini tuna wachezaji bora kuliko Hispania kwa sasa. Inaweza kusikika kama upuuzi, lakini ninaamini hivyo tukitazama uwezo binafsi wa kila mchezaji. Tatizo letu kubwa si la Kombe hili la Dunia pekee, bali tumekuwa hatuchezaji kama timu. Wachezaji wengi wanaonekana kujali zaidi viwango vyao binafsi kuliko timu nzima.”
Tuchel anaondoka?
Kando na kuzungumzia ubora wa wachezaji, Scholes amemlenga moja kwa moja kocha wa England, Thomas Tuchel. Kwa mtazamo wa Scholes, inaonekana Tuchel anajaribu kutengeneza mazingira ya kuondoka kufuatia matokeo ya timu hiyo kwenye Kombe la Dunia.
Scholes anaamini kuwa historia ya Tuchel katika klabu alizopita, kama vile PSG, Borussia Dortmund, na Bayern Munich, inaashiria kuwa huwa ana tabia ya kugombana na watu na hatimaye kulazimisha kuondoka. Kwa sasa, Scholes anaona kuwa huenda kocha huyo anapita katika njia hiyo hiyo akiwa na timu ya taifa ya England.
Nani mrithi wa Tuchel?
Kufuatia tetesi za kuondoka kwa Tuchel, majina kadhaa yameanza kuhusishwa na kiti hicho, ikiwemo Ole Gunnar Solskjaer. Hata hivyo, Scholes na mwenzake wa zamani Nicky Butt hawajaonyesha kuunga mkono wazo la Solskjaer kuinoa England.
Butt alisema: “Simuoni kama kocha wa England. Bila kumvunjia heshima, sidhani kama yupo katika daraja hilo la kuifundisha timu ya taifa. England inapaswa kutafuta kocha bora zaidi anayepatikana sokoni sasa hivi.”
England imemaliza mashindano haya katika nafasi ya tatu baada ya kuifunga Ufaransa 6-4, huku Hispania ikitawazwa kuwa mabingwa wa dunia baada ya kuichapa Argentina 1-0 katika fainali.