Skip to content

Real Madrid yafunga mlango kwa Zubimendi; Man City yamnyakua Jeremy Monga

SokaNews
Updated: Published: Jumamosi, 11 Julai 2026 · 2 min read
realmadrid arsenal manchestercity martinzubimendi jeremymonga usajili
Real Madrid yafunga mlango kwa Zubimendi; Man City yamnyakua Jeremy Monga

Real Madrid yafunga mlango kwa Zubimendi

Matumaini ya Real Madrid kumsajili kiungo wa Arsenal, Martin Zubimendi, yameonekana kufutika baada ya ripoti nchini Hispania kuashiria kuwa klabu hiyo haifikirii kufanya jaribio lolote la kumpata mchezaji huyo msimu huu.

Zubimendi, ambaye alikuwa nguzo muhimu katika kikosi cha Mikel Arteta kilichotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (Premier League) msimu uliopita, alihusishwa sana na mpango wa kurejea nchini Hispania kujiunga na miamba hiyo ya Madrid. Hata hivyo, mwandishi wa habari Alberto Pereiro ameweka wazi kuwa dili hilo haliwezi kutokea.

Katika majibu yake kwa shabiki mmoja kupitia mtandao wa X, Pereiro alisisitiza kuwa kiungo huyo alikumbwa na changamoto nyingi mwishoni mwa msimu uliopita na anatarajiwa kuwa na wakati mgumu zaidi msimu ujao, jambo linalofanya uwezekano wa uhamisho huo kuwa mdogo sana.

Arsenal inaendelea kumuamini Zubimendi kama sehemu ya msingi ya mipango yao, huku kocha Mikel Arteta akiripotiwa kutafuta kiungo mwingine wa kusaidiana naye na Declan Rice, ambapo jina la Bruno Guimaraes wa Newcastle United likitajwa kama chaguo bora zaidi.

Man City yamnyakua Jeremy Monga

Wakati huo huo, Arsenal imepata pigo katika harakati zao za kusajili vipaji vipya baada ya kupitwa na Manchester City katika kinyang’anyiro cha kumsajili winga kinda wa Leicester City, Jeremy Monga.

Monga, mwenye umri wa miaka 17, ametua rasmi katika klabu ya Manchester City baada ya mabingwa hao wa pili wa Ligi Kuu ya England kuweka ofa bora zaidi kuliko ile ya Arsenal. Mchezaji huyo ameeleza furaha yake kubwa kujiunga na klabu hiyo.

“Nilipofahamu kuwa Manchester City wana shida na mimi, nilijua mara moja kuwa huu ndio uamuzi sahihi kwangu. Kwa mchezaji yeyote kijana, kuwa sehemu ya klabu hii kubwa ni ndoto iliyotimia,” alisema Monga.

Monga aliongeza kuwa kuvutiwa kwake na jinsi klabu hiyo inavyowapa nafasi vijana kutoka akademi yao, kama ilivyo kwa Phil Foden na Nico O’Reilly, kulimfanya aone City ndiyo sehemu sahihi ya kukuza kipaji chake.

Mkurugenzi wa soka wa Manchester City, Hugo Viana, amesema kuwa klabu hiyo imekuwa ikimfuatilia Monga kwa muda mrefu na wanaamini kuwa ana uwezo mkubwa wa kuendelea kukua na kufika mbali zaidi chini ya maelekezo yao.