Skip to content

Richarlison na Tottenham: Uhusiano unazidi kuvunjika

SokaNews
Updated: Published: Jumamosi, 12 Septemba 2026 · 2 min read
tottenham richarlison harrykane bayernmunich usajili premierleague
Richarlison na Tottenham: Uhusiano unazidi kuvunjika

Mgogoro wa Richarlison na Spurs

Uhusiano kati ya mshambuliaji wa Brazil, Richarlison, na klabu yake ya Tottenham Hotspur unaonekana kufika pabaya. Mchambuzi wa masuala ya usajili, Fabrizio Romano, amebainisha kuwa hali si shwari na uhusiano huo unaonekana ‘kuvunjika kabisa’.

Katika kipindi cha wiki za hivi karibuni, Richarlison amekuwa kwenye sintofahamu kubwa kuhusu hatma yake kufuatia dili mbalimbali za kumuondoa klabuni hapo kugonga mwamba. Miongoni mwa matukio hayo ni jaribio la Tottenham kumtumia mchezaji huyo katika makubaliano ya kumsajili Iliman Ndiaye kutoka Everton, jambo ambalo lilishindikana baada ya Richarlison kushindwa kukubaliana na timu hiyo ya Goodison Park.

Changamoto ya Mkataba

Ripoti zinaeleza kuwa kuna mgogoro unaoendelea kuhusu miezi tisa iliyosalia kwenye mkataba wake wa sasa. Richarlison anaripotiwa kutaka kuvunja mkataba wake na kuondoka kama mchezaji huru, jambo ambalo Tottenham hawapo tayari kulikubali. Klabu hiyo ina chaguo la kuongeza mkataba wake kwa miezi mingine 12, hali inayofanya mazungumzo kuwa magumu.

“Kwa sasa, uhusiano na Tottenham unaonekana kuvunjika kabisa,” alisema Fabrizio Romano kwenye chaneli yake ya YouTube.

Awali, klabu ya Trabzonspor ya Uturuki ilikuwa na nia ya dhati ya kumsajili mshambuliaji huyo, na hata Richarlison alifikia makubaliano nao, lakini Tottenham walikataa ofa zote zilizowasilishwa. Kwa sasa, kuna taarifa za kuhusishwa na klabu ya Vasco da Gama ya nchini kwao Brazil, ingawa Romano amesisitiza kuwa hakuna chochote cha karibu kilichofikiwa kati ya pande hizo mbili.

Harry Kane na Bayern Munich

Katika upande mwingine, hadithi ya mchezaji wa zamani wa Spurs, Harry Kane, inaendelea nchini Ujerumani. Nahodha huyo wa England yupo kwenye mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya na klabu yake ya Bayern Munich.

Romano aliongeza kuwa mazungumzo hayo yanaendelea vizuri ingawa hayatakamilika haraka. “Bayern wameipa kipaumbele cha juu sana suala la mkataba mpya wa Harry Kane, na kisha Michael Olise. Mazungumzo yanaendelea na Bayern wako tayari kumpa ofa muhimu sana,” alihitimisha mchambuzi huyo.