Peter Schmeichel ammwagia sifa tele Marcus Rashford baada ya kiwango bora dhidi ya Everton
Uamsho wa Rashford chini ya Carrick
Mkongwe wa Manchester United, Peter Schmeichel, ametoa pongezi za dhati kwa mshambuliaji Marcus Rashford baada ya kuonyesha kiwango cha kuvutia katika mchezo wa sare ya 2-2 dhidi ya Everton siku ya Jumapili.
Rashford, ambaye alikuwa akihusishwa na kuondoka klabuni hapo baada ya msimu uliopita kucheza kwa mkopo Barcelona, alionekana kama yupo kwenye njia ya kutokea chini ya kocha wa zamani, Ruben Amorim. Hata hivyo, chini ya kocha mpya Michael Carrick, mchezaji huyo amerejeshwa kikosini na kuonyesha kuwa bado ana mchango mkubwa.
Ushirikiano wa aina yake na Luke Shaw
Katika mchezo huo dhidi ya Everton, Rashford alionekana kurudisha makali yake, hususan katika ushirikiano wake na beki wa kushoto Luke Shaw. Wawili hao walionyesha maelewano mazuri ambayo yalimfurahisha hata Wayne Rooney, ambaye alikuwa akitazama mchezo huo.
Kocha Michael Carrick naye hakusita kuwapongeza wawili hao kwa kazi waliyoifanya uwanjani:
“Marcus na Luke walikuwa hatari sana upande huo. Wamecheza pamoja kwa muda mrefu sasa na wanaelewana. Tunajaribu kujenga ushirikiano na mchanganyiko sahihi kote uwanjani.”
Tatoo inayozua gumzo: Ishara ya dhamira
Peter Schmeichel anaamini kuwa Rashford yupo tayari kupambana msimu huu, akisisitiza kuwa hata tatoo mpya aliyochora mchezaji huyo ni ishara tosha ya nia yake ya kurejea kwenye ubora wake wa zamani.
Schmeichel alisema:
“Rashford sasa anafanya mambo vizuri. Nadhani alikuwa mzuri sana. Kuna taarifa za tatoo yake mpya ambayo ameandika namba zote za jezi alizowahi kuvaa na kuongeza namba 9 [namba yake mpya ya jezi]. Hii inaonyesha dhamira yake ya kurejea kama alivyokuwa miaka minne iliyopita alipofunga mabao 30 kwa msimu mmoja.”
Gwiji huyo aliongeza kuwa Rashford hakuwa akijaribu kufanya kila kitu peke yake, bali alicheza kwa akili na kuwasaidia wenzake, jambo ambalo ni ishara ya ukomavu na hamu ya kuisaidia klabu hiyo.
“Huyu ndiye Marcus Rashford tunayetamani kumuona. Ikiwa hivi ndivyo atakavyocheza msimu huu, basi tunasema karibu tena Marcus, tulikumiss!” alihitimisha Schmeichel.