Skip to content

Thomas Tuchel alinusurika kufutwa kazi baada ya ushindi dhidi ya DR Congo

SokaNews
Updated: Published: Ijumaa, 3 Julai 2026 · 2 min read
thomastuchel england worldcup drcongo harrykane fa
Thomas Tuchel alinusurika kufutwa kazi baada ya ushindi dhidi ya DR Congo

Shinikizo kwa Tuchel lilikuwa kubwa

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya England, Thomas Tuchel, alikuwa kwenye wakati mgumu sana kuelekea mchezo wa hatua ya 32 bora ya Kombe la Dunia dhidi ya DR Congo. Ripoti zinaeleza kuwa iwapo England ingepoteza mchezo huo, Tuchel angekuwa katika hatari kubwa ya kufutwa kazi.

England ilikuwa nyuma kwa muda mrefu na ilikuwa imesalia na dakika 15 pekee mchezo kumalizika wakiwa bado wako nyuma, jambo ambalo lingekuwa moja ya matokeo mabaya zaidi katika historia ya soka la nchi hiyo kwenye Kombe la Dunia. Uongozi wa Shirikisho la Soka la England (FA) ulimleta Mjerumani huyo kwa lengo kuu la kutwaa taji la dunia, hivyo kushindwa mbele ya DR Congo kungechukuliwa kama jambo lisilokubalika.

Uokozi wa Harry Kane

Nahodha Harry Kane ndiye aliyekuwa mwokozi wa Tuchel katika mchezo huo. Mabao mawili ya lulu ya Kane yaliipa England ushindi na kuivusha kwenda hatua ya 16 bora, ambako sasa watakutana na wenyeji Mexico katika Uwanja wa Azteca.

Ushindi huo umempa ahueni kubwa Tuchel, na ripoti za karibu zinasema kuwa kwa sasa nafasi yake ni salama bila kujali matokeo yatakayotokea katika mchezo ujao dhidi ya Mexico. FA wanaamini kuwa kulingana na ugumu wa michuano hii na ubora wa timu zinazoshiriki, kocha huyo anapaswa kuendelea na majukumu yake ili kuijenga timu hiyo kuelekea hatua nyingine.

Hali ya kikosi na majeruhi

Kuelekea mchezo dhidi ya Mexico, Tuchel anapata nafuu kutokana na hali za wachezaji wake kurejea vyema. Katika mchezo uliopita dhidi ya DR Congo, kocha huyo alikosa huduma za Jarell Quansah na Reece James, jambo lilimlazimisha kumpanga Djed Spence katika nafasi ya beki wa kulia.

Akizungumzia hali ya wachezaji hao, Tuchel alisema:

Wanaendelea vizuri na wako karibu zaidi kurejea uwanjani. Nilikuwaona wakifanya mazoezi uwanjani. Kwa asili ya majeraha yao, Jarell yuko mbele kidogo ya Reecey. Tutahakikisha wako fiti kwa ajili ya mechi zijazo.

Ingawa bado haijafahamika kama wataanza dhidi ya Mexico, kurejea kwao kutakuwa na mchango mkubwa iwapo England itafanikiwa kutinga hatua ya robo fainali, ambako wanaweza kukutana na Brazil au Norway.