Skip to content

Troy Deeney awashambulia mastaa wa Arsenal baada ya ushindi wa England dhidi ya Panama

SokaNews
Updated: Published: Jumapili, 28 Juni 2026 · 2 min read
england arsenal bukayosaka nonimadueke troydeeney kombeladunia
Troy Deeney awashambulia mastaa wa Arsenal baada ya ushindi wa England dhidi ya Panama

Mchambuzi atoa neno zito kwa mawinga wa England

Aliyekuwa mshambuliaji wa Ligi Kuu ya England, Troy Deeney, ametoa shutuma nzito kwa mawinga wa timu ya taifa ya England baada ya mchezo wa Kombe la Dunia dhidi ya Panama, ambao England walishinda 2-0.

Licha ya England kufanikiwa kupata ushindi huo na kufuzu hatua inayofuata, Deeney hakuona sababu ya kupongeza kiwango kilichoonyeshwa na mawinga wake, akiwemo Bukayo Saka na Noni Madueke wa Arsenal, pamoja na Marcus Rashford.

Takwimu mbovu zawaangusha

Akizungumza kupitia CBS Sports, Deeney alionyesha kukerwa na kiasi cha mipira iliyopotea (possession lost) wakati wa mchezo huo. Saka alipoteza mipira 14, Rashford 20, huku Madueke akipoteza mipira 7.

“Ni sawa kupoteza mipira kama unafanya vitu vya kiufundi na pasi za hatari. Lakini kama unafanya hivyo bila ufanisi, ni tatizo. Madueke alipoingia, alijaribu kukimbiza mpira lakini akajikuta anautoa nje ya uwanja. Hicho ni kitu cha kunifurahisha?”

Deeney aliongeza kuwa mchezo huo ulikuwa wa hovyo hasa katika kipindi cha pili, wakati ambapo Panama ilijiamini zaidi na kuacha nafasi wazi, lakini mawinga wa England walishindwa kuzitumia.

”Wana kiburi na wajinga”

Uchambuzi wa Deeney ulikuwa mkali zaidi alipoelezea mtazamo wake kuhusu wachezaji hao. Alidai kuwa tatizo kubwa ni mtazamo wa wachezaji wengi wa England wanapokutana na timu zinazochukuliwa kuwa ndogo.

“Unajua walikuwa wakoje? Walikuwa na kiburi na ujinga. Walidhani wanachotakiwa kufanya ni kukimbia tu kupita mabeki wa upinzani kwa sababu tu wanacheza katika vilabu vikubwa. Hapana, unacheza na mtu mwingine ambaye anaiwakilisha nchi yake na anataka kuonyesha uwezo wake mbele ya dunia nzima.”

Harry Kane na Bellingham ndio tumaini la England

Katika upande mwingine, Danny Murphy ameipongeza safu ya ushambuliaji ya England, akisisitiza kuwa Jude Bellingham na nahodha Harry Kane ndio nguzo kuu zinazoifanya England kuwa na matumaini ya kutwaa taji hilo.

Murphy amemweleza Kane kama mfungaji bora wa muda wote ambaye kila anapocheza, matarajio ya kufunga ni makubwa. Pamoja na malalamiko ya Deeney kwa mawinga, ushindi huu umeipeleka England kukutana na DR Congo katika hatua ya 32 bora ya michuano hiyo ya Kombe la Dunia.