Skip to content

Chelsea wamnasa Joao Pedro, wafungua ukurasa mpya wa usajili kwa Pep Chavarria

SokaNews
Updated: Published: Jumapili, 2 Agosti 2026 · 2 min read
chelsea joaopedro pepchavarria usajili premierleague xabialonso
Chelsea wamnasa Joao Pedro, wafungua ukurasa mpya wa usajili kwa Pep Chavarria

Joao Pedro kusalia Stamford Bridge

Klabu ya Chelsea imefanikiwa kuwakatisha tamaa wapinzani wao katika Ligi Kuu ya England, Arsenal, baada ya kufikia makubaliano ya kumuongezea mkataba mpya nyota wao Joao Pedro. Mshambuliaji huyu raia wa Brazil alikuwa nguzo muhimu katika kikosi hicho msimu uliopita, hali iliyozua mvuto kwa klabu mbalimbali kubwa barani Ulaya.

Mwandishi wa habari za usajili, Nicolo Schira, amethibitisha kuwa Pedro amekubali kusaini mkataba mpya utakaomfanya awepo klabuni hapo hadi mwaka 2033, ukiwa na kipengele cha kuongeza muda. Mkataba huu mpya pia unakuja na ongezeko kubwa la mshahara, hatua inayolenga kumuonyesha thamani yake.

“Done Deal! Joao Pedro yuko tayari kuongeza mkataba wake na Chelsea hadi 2033, na atapokea ongezeko kubwa la mshahara. Chelsea wamekataa ofa za PSG, Barcelona, na Arsenal katika wiki za hivi karibuni kwa mshambuliaji huyu wa Brazil, ambaye sasa anaonekana kama mchezaji ambaye hauzwi,” alieleza Schira kupitia mtandao wa X.

Chelsea wakaribia kumnasa Pep Chavarria

Baada ya kukamilisha usajili wa Danny Welbeck na kuelekea kumpata Jordan Henderson, kikosi cha kocha Xabi Alonso sasa kimejikita kwenye kuimarisha safu ya ulinzi. Beki wa kushoto wa Rayo Vallecano, Pep Chavarria, ndiye anayepigiwa upatu kuwa mbadala sahihi wa Marc Cucurella aliyeondoka klabuni hapo.

Awali mazungumzo kati ya klabu hizo mbili yalikuwa yamekwama kutokana na Chelsea kukataa kulipa dau kubwa lisilo la lazima. Hata hivyo, ripoti za hivi karibuni kutoka kwa mtaalamu wa usajili Fabrizio Romano zinaashiria kuwa upepo umebadilika.

“Chelsea wametuma ofa mpya leo kwa Rayo Vallecano kwa ajili ya Pep Chavarria. Mazungumzo yanaendelea na Chelsea wapo makini hadi dakika ya mwisho kwani mchakato huu umekuwa mgumu zaidi ya ilivyotarajiwa,” alisema Romano.

Romano aliongeza kuwa mchezaji mwenyewe anashinikiza dili hilo likamilike kwani ana hamu kubwa ya kujiunga na miamba hiyo ya London. Licha ya kuwa dili hilo halijakamilika rasmi, kuna matumaini makubwa kuwa pande zote zitafikia muafaka hivi karibuni.

Chelsea wamekuwa na shughuli pevu katika dirisha hili la usajili huku wakipunguza idadi ya wachezaji ili kuweka uwiano mzuri wa kifedha. Hadi sasa, wamefanikiwa kupata takriban £113m kupitia mauzo ya wachezaji mbalimbali kama Marc Cucurella, Alejandro Garnacho, Andrey Santos, na Tyrique George.