Skip to content

Fabrizio Romano afunguka kuhusu taarifa za Marcus Rashford kutaka kujiunga na Fenerbahce

SokaNews
Updated: Published: Jumatano, 15 Julai 2026 · 2 min read
marcusrashford manchesterunited fenerbahce usajili fabrizioromano
Fabrizio Romano afunguka kuhusu taarifa za Marcus Rashford kutaka kujiunga na Fenerbahce

Uvumi wa Rashford kwenda Uturuki hauna ukweli

Kumekuwa na taarifa nyingi zikisambaa katika vyombo vya habari vya Uturuki zikidai kuwa klabu ya Fenerbahce inafanya jitihada kubwa za kumsajili mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford. Inadaiwa kuwa klabu hiyo ya Super Lig ina nia ya kumjumuisha Rashford katika kikosi chao baada ya awali kufanikiwa kumsajili Mason Greenwood.

Taarifa hizo zilidai kuwa viongozi wa Fenerbahce walikuwa wameelekea jijini Manchester ili kuanza mazungumzo rasmi na klabu hiyo ya Uingereza kwa ajili ya kupata saini ya winga huyo. Hata hivyo, mtaalamu wa masuala ya usajili barani Ulaya, Fabrizio Romano, amejitokeza na kufafanua hali halisi.

Hakuna mazungumzo yanayoendelea

Kupitia chaneli yake ya YouTube, Romano ameweka bayana kuwa taarifa zinazohusisha Rashford na Fenerbahce hazina ukweli wowote. Alisisitiza kuwa hakuna mawasiliano ya aina yoyote yaliyofanyika kati ya pande hizo mbili.

“Ripoti ni nyingi jamani, lakini ninachofahamu ni kwamba hakuna chochote kinachoendelea kati ya Marcus Rashford na Fenerbahce. Hakuna mazungumzo, hakuna majadiliano, na hiyo ni kwa sababu Marcus Rashford, kwa heshima zote kwa Fenerbahce, hafikirii kuhamia Uturuki katika hatua hii ya maisha yake ya soka.”

Focus ipo kwenye Kombe la Dunia na Man Utd

Kwa sasa, Rashford yuko bize akiitumikia timu yake ya taifa katika michuano ya Kombe la Dunia. Kulingana na Romano, baada ya michuano hiyo kumalizika, mchezaji huyo atarejea Manchester United kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya (pre-season).

Kocha wa Manchester United, Michael Carrick, anatarajiwa kufanya kazi na Rashford wakati wa kambi hiyo ya mazoezi ili kutathmini kiwango chake na nidhamu yake kabla ya kufanya maamuzi ya mwisho kuhusu hatima yake ndani ya klabu hiyo mwezi Agosti.

“Rashford anajikita kwenye Kombe la Dunia. Baada ya hapo, atatathmini hali yake ndani ya Manchester United. Atashiriki pre-season, na kocha Michael Carrick anatarajia kufanya naye kazi ili kuona hisia zake na mtazamo wake kabla ya kuamua kama atabaki au ataondoka,” aliongeza Romano.

Kwa sasa, mashabiki wa Manchester United wanaweza kutulia kwani hakuna makubaliano yoyote yanayompeleka nyota huyo nchini Uturuki, na kila kitu kitajulikana zaidi mara baada ya mchezaji huyo kumaliza majukumu yake ya kimataifa na kuanza mazoezi na klabu yake.