Manchester City kupania kumsajili Enzo Fernandez kutoka Chelsea
Man City wanataka kuongeza kasi ya usajili
Manchester City wameripotiwa kuwa mbioni kuongeza kasi katika jitihada zao za kumsajili kiungo wa Chelsea, Enzo Fernandez, katika siku chache zijazo. Ingawa hadi sasa hakujawa na mazungumzo rasmi baina ya klabu hizo mbili, taarifa zinaonyesha kuwa mabingwa hao wa England bado wanafuatilia kwa karibu hali ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina.
Hali ilivyo sasa
Licha ya Chelsea kuweka muda wa mwisho wa klabu hiyo kufanya ofa rasmi ambao ulipita wiki iliyopita bila Man City kuingia sokoni, mwandishi wa habari za usajili Fabrizio Romano amethibitisha kuwa mawasiliano kati ya City na wakala wa mchezaji huyo, Javier Pastore, bado yanaendelea. Hii inaashiria kuwa City bado wana shauku ya kumpata kiungo huyo.
Akizungumzia hali hiyo, mwandishi Pete O’Rourke kutoka Football Insider amedai kuwa mambo yanatarajiwa kupamba moto hivi karibuni:
“Nataraifa kuwa mambo yataongezeka kasi katika jitihada za Man City kumsajili Enzo Fernandez katika siku chache zijazo. Tunajua City wana nia naye na tunajua Chelsea hawajafunga mlango wa kumuuza ikiwa bei itakuwa sahihi.”
Changamoto ya makubaliano
Ingawa mchezaji mwenyewe anaonekana kuwa kwenye rada za City, kikwazo kikubwa bado ni makubaliano kati ya klabu hizo mbili. Chelsea hapo awali walikuwa wameweka bei ya paundi milioni 120 kama kifungu cha kuruhusu mchezaji huyo kuondoka, lakini kwa sasa muda huo wa makubaliano ya mdomo umepita, hali inayomaanisha kuwa kila kitu kiko mikononi mwa Chelsea.
Manchester City kwa sasa wako kwenye mchakato wa kusuka upya kikosi chao baada ya kuondokewa na wachezaji kadhaa katika dirisha hili la usajili, na Enzo anatajwa kuwa miongoni mwa majina yanayoweza kuongeza nguvu kwenye eneo la kiungo.
Taarifa nyingine kutoka Stamford Bridge
Wakati sakata la Enzo likiendelea, klabu ya Chelsea pia ipo katika hatua za mwisho za kumpeleka mshambuliaji Nicolas Jackson kwa mkopo katika klabu ya Atletico Madrid. Mkurugenzi wa michezo wa Atletico, Mateu Alemany, anadaiwa kusafiri kuelekea London ili kukamilisha dili hilo ambalo litamfanya Jackson aungane na safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo ya Uhispania.