Skip to content

Nagelsmann awaka baada ya wachezaji wake kudai Ecuador walitaka ushindi zaidi

SokaNews
Updated: Published: Ijumaa, 26 Juni 2026 · 2 min read
ujerumani juliannagelsmann ecuador kombeladunia joshuakimmich jamalmusiala
Nagelsmann awaka baada ya wachezaji wake kudai Ecuador walitaka ushindi zaidi

Ujerumani yachapwa, Nagelsmann akataa lawama za wachezaji

Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani, Julian Nagelsmann, ametoa maneno makali kufuatia kichapo cha mabao 2-1 walichokipata kutoka kwa Ecuador kwenye mchezo wa hatua ya makundi ya Kombe la Dunia. Ujerumani ilianza vyema kwa kupata bao la mapema kupitia kwa Leroy Sane, lakini Ecuador walirudi mchezoni na kupindua meza kibabe.

Baada ya mchezo huo, baadhi ya wachezaji muhimu wa Ujerumani walionekana kukiri kuwa walizidiwa kiu ya ushindi na wapinzani wao. Hata hivyo, Nagelsmann hakuwa tayari kukubaliana na mtazamo huo, akielezea madai hayo kama kitu kisicho na msingi.

Wachezaji wakiri kuzidiwa kiu ya ushindi

Nahodha Joshua Kimmich alikuwa miongoni mwa wachezaji walioonyesha wazi kutoridhishwa na kiwango chao, akisema kuwa mazingira ya uwanjani yalikuwa mazuri lakini walishindwa kukabiliana na nguvu za wapinzani wao.

“Tofauti ya leo ilikuwa kwamba wapinzani wetu walitaka ushindi zaidi kuliko sisi, na hilo lilijionyesha hasa kipindi cha pili. Ndiio maana wameshinda, tena kwa haki kabisa,” alisema Kimmich.

Kauli hii iliungwa mkono na washambuliaji Deniz Undav na Jamal Musiala, ambao wote walikiri kuwa Ecuador walikuwa na njaa kubwa zaidi ya matokeo na walicheza kwa nguvu na umakini mkubwa kuliko kikosi chao.

”Ni upuuzi mtupu” - Nagelsmann

Kauli hizo za wachezaji zilionekana kumkera kocha Nagelsmann, ambaye alikanusha vikali kuwa wachezaji wake walikosa utayari wa kupambana. Kwa mujibu wa kocha huyo, ni makosa kudai kuwa timu haikutoa kila kitu uwanjani.

“Ecuador walitaka ushindi zaidi kuliko sisi? Huo ni upuuzi. Tafadhali acheni huu upuuzi, kweli kabisa. Kwani vijana hawakutoa kila kitu leo?” alihoji Nagelsmann.

Kocha huyo aliongeza kuwa Ecuador walicheza kwa hatari zaidi na kuchukua maamuzi magumu uwanjani. Alisisitiza kuwa mabadiliko ya kikosi aliyoyafanya yalitokana na mikakati ya mchezo, lakini kamwe hawezi kukubali kuwa wachezaji wake hawakuonyesha jitihada. Kwake yeye, kuwalaumu wachezaji kwa kukosa njaa ya ushindi ni tafsiri rahisi sana ya mchezo uliokuwa na changamoto za kiufundi.